Tuchel : Uchovu wa Wachezaji Ndio Sababu.

Meneja Thomas Tuchel amekiri hakuna furaha kwa Chelsea baada ya klabu hiyo kushindwa kushinda mechi ya ligi kwa mara ya sita katika mechi saba zilizopita siku ya Jumanne katika sare ya 1-1 na Brighton.

 

“[Hata] katika majibu ya bao [tulilofunga], unaweza kuona kwamba tumechoka,” Tuchel aliiambia BT Sport. “Tumefarijika lakini hakuna furaha.

“Tunaonekana tumechoka, na tumechoka …. Unaweza kuona tumechoka kiakili. Tunahitaji siku kadhaa za kupumzika, hakuna suluhisho lingine.”

Kuhusu Lukaku na Ziyech kuonekana wakigombana wakati wa mapumziko, alisema: “Ni kawaida kwamba wao [Ziyech na Lukaku] wanazungumza, ni kawaida kwamba hawana furaha.”

Hakim Ziyech alianza kuifungia Chelsea dakika ya 28, lakini Adam Webster wa Brighton aliisawazishia timu yake bao la kwanza kipindi cha pili na kupata pointi moja.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe