Yanga imewaita wachezaji 19 watakaoingia kambini katika kujiandaa na mashindano ya Kagame ambapo katika hao kutakuwa na mastaa wawili wapya Dickson Ambundo na beki David Brayson.
Yanga itawatumia pia wachezaji sita wazoefu wakiongozwa na nahodha wao msaidizi, kiungo Mukoko Tonombe ambaye amewaambia mabosi wake hatarudi nyumbani na atabaki kuitumikia.
Mbali na Mukoko, wengine ni Kabwili, Paul Godfrey ‘Boxer’, Dickson Job, Zawadi Mauya, na Waziri Shentembo.
Mastaa hao watachanganyika na vijana chini ya miaka 20 ambao ni kipa Geofrey Magaigwa, mabeki M Msenda, Said Mashoto, R Msonjo na Ally Said, viungo Omary Chibada, S Kwangala, J Guber, Best Kahemela na washambuliaji Abby Mikimba, A Yunus.
SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!



Angelina
Kila kheri yanga