Cody Gakpo amesema Uholanzi inaweza kufanya vyema zaidi baada ya bao lake la la kwanza  lililowasaidia timu hiyo kushinda 2-0 kabla ya bao la dakika za mwisho la Klaassen dhidi ya Senegal katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia.

 

Gakpo: "Uholanzi Inaweza Kufanya Vizuri Zaidi"

Gakpo wa PSV  ndiye aliyewafungulia njia ya kupata alama tatu katika mchezo wa jana baada ya kwenda kipindi cha kwanza kuisha kwa bila kufungana, huku Simba wa teranga wakionekana kucheza kwa ubora na kupiga mashuti yaliyolenga lango manne.


Inaashiria kurejea kwa ushindi kwenye Kombe la Dunia kwa kikosi cha Louis van Gaal, ambaye alikosa mchuano uliopita nchini Urusi, lakini licha ya kuanza kwa ushindi katika kundi A, Gakpo anahisi kuna nafasi ya kuboreshwa baada ya mechi ya jana.

Mchezaji huyo alimwambia mtangazaji wa NOS kuwa; “Nafikiri tunaweza kufanya vyema zaidi. Tulikuwa wazuri katika umiliki wetu hivyo tunapaswa kuchanganua hili ipasavyo na kuchukua pointi nzuri kwenye mchezo unaofuata.”

Gakpo: "Uholanzi Inaweza Kufanya Vizuri Zaidi"

Mchezo huo ulikuwa mgumu baada ya timu hizo kwenda kipindi cha kwanza bila kufungana licha ya kila timu kupeleka mashambulizi kwa mwenzake na hawakutofautiana sana kwenye umiliki wa mpira.

Gakpo: "Uholanzi Inaweza Kufanya Vizuri Zaidi"

Uholanzi wanasema kuwa kama timu hawakuwa vizuri, lakini bado wanaweza kutafuta njia kueleka mchezo unaofuata ili washinde, pia waliongeza wanaweza kufika mbali sana na kuwa mabingwa wa Dunia na si vinginevyo.


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa