Aubameyang Mali Rasmi ya Chelsea

Klabu ya Chelsea imekamilisha usajili wa Pierre- Emerick Aubameyang kutoka Barcelona kwa dau la £10.3M. Aubameyang ambaye alikuwa ni mshambuliaji wa zamani wa Arsenal amesaini kandarasi ya miaka miwili  kuitumikia Chelsea.

Aubameyang Mali Rasmi ya Chelsea

Mchezaji huyo alijiunga na vijana wa Xhavi Hernandez msimu uliopita ambapo alianza vizuri klabuni hapo lakini baada ya usajili wa Roberto Lewandowski na uhaba wa fedha ambao Barcelona wanao waliona wamuuze kwani sasa wameshapata mshambuliaji wa daraja la juu kabisa.

Aubameyang ni Mgabon mwenye umri wa miaka 33 anaenda kuungana na vijana wa darajani. Chelsea misimu miwili wamesajili washambuliaji akiwemo Romelu Lukaku kutoka Intermillan ambaye hakufanikiwa sana na kumrudisha kwa mkopo Inter, lakini pia kumpeleka Werner RB.

Aubameyang Mali Rasmi ya Chelsea

Msimu huu Chelsea imeanza msimu kwa kusuasua kutokana na kukosa watu sahihi kwenye muda sahihi kupoteza nafasi za wazi za magoli imekuwa ni sugu wa The Blues hivyo wamemleta mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuchukua kiatu cha ufungaji bora England, huenda akaongeza kitu.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.