Pierre Emerick Aubameyang amekaribia kujiunga na klabu ya Chelsea yenye maskani yake jijini London akitokea klabu ya Fc Barcelona.
Mchezaji huyo ambaye alijiunga ana klabu ya Barcelona mwezi Januari mwaka huu akitokea klabu ya Arsenal ambapo alicheza kwa misimu kadhaa.

Aubameyang anaamua kutimkia Chelsea hii ni baada ya ujio wa mshambuliaji Roberto Lewandowski aliejiunga klabuni hapo akitokea klabu ya Bayern Munchen ya nchini Ujerumani hali iliyomfanya mchezaji huyo kuona ufinyu wa nafasi yake ndani ya kikosi hicho na kuamua kutafuta changamoto upande mwingine.
Klabu ya Chelsea ipo kwenye hatua za mwisho na wababe wa Catalan kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo hatari kwa kiasi cha € milioni 10 pamoja na beki wa kushoto wa Chelsea Marcos Alonso ambae atatimkia Barcelona kama sehemu ya malipo ya Aubameyang.

