Haaland Azidi Kung'ara EPL.

Mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland anazidi kufanya makubwa katika ligi kuu ya England baada ya kufunga hattrick mara mbili mfululizo akiwa ndio mchezaji wa kwanza kufanya hivyo toka ligi iliporejea.

Haaland Azidi Kung'ara EPL.

Haaland amefanya hivyo kwenye mchezo uliopita dhidi ya Crystal Palace ambao ulimalizika kwa City kushinda mabao manne kwa mawili, na jana ambapo walichecheza dhidi ya Nottingham Forest huku kabla ya mapumziko alikuwa ameshafunga mabao matatu, Mchezo uliomalizika kwa wao kushinda mabao 6-0.

Mchezaji huyo ameweka historia katika ligi kuu kwani amefunga mabao mengi baada ya mechi tano mabao zaidi ya timu 15 za Premier League. Mpaka sasa Haaland amecheza mechi 5 na amefunga mabao 9 akiwa ni kinara wa wafungaji mpaka sasa.

Haaland Azidi Kung'ara EPL.

Vijana wa Pep Guardiola ambao ndio mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Englang  wapo nafasi ya pili kwenye msimamo huku wakiwa tofauti yao na aliyepo nafasi ya kwanza ambaye ni Arsenal ikiwa ni alama mbili tuu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.