Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandez amewashukuru mashabiki zao kwa kusafiri mpaka Leicester kwaajili ya kuwapa ushirikiano wa kushangilia.

Bruno kupitia ukurasa wake wa Twitter ameposti ujumbe uliosomeka hivi;
“Alama tatu nyingine tukiwa ugenini, shukrani nyingi na za pekee kwa mashabiki waliosafiri nasi mpaka Leicester wenye hali ya hewa nzuri, sasa ni muda wa kuimarika na kurejea tena siku ya Jumapili”

Man Utd walikuwa ugenini dhidi ya Leicester City ambapo walipata ushindi mgumu wa bao 1-0, goli lililofungwa na Jardon Sancho aliyepokea pasi mujarabu kutoka kwa Marcus Rashford mnamo dakika ya 23, bao lililodumu mpaka filimbi ya mwisho ya mwamuzi.

Ushindi huo unakuwa ni wa tatu mfululizo kwa Man utd baada ya kushinda dhidi ya Liverpool, wakashinda tena mbele ya Southampton na ule wa jana ukakamilisha rekodi ya ushindi kwenye mechi 3 mfululizo.
Mchezo unaofuata watakutana na Arsenal waliopo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi ya Uingereza ambao hawajapoteza mechi hata moja.

