Klabu ya OG Nice ya nchini Ufaransa imemsajili kiungo mshambuliaji Ross Barkley kwa uhamisho huru kutoka Chelsea. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 katika msimu huu hajapata nafasi ya kuanza katika kikosi cha Thomas Tuchel.

Ross Barkley ambaye msimu uliopita alitolewa kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa,baada ya msimu kuisha amerudi klabuni japokuwa kutokana na ufinyu wa kupata namba katika kikosi cha kwanza hata katika wachezaji wa ziada kukosekana imebidi asitishe mkataba na The Blues.
Kandarasi ya kusitisha mkataba baina yake na Chelsea ilifanyika siku chache zilizopita ambapo timu hiyo iliona haina haja ya kuendelea nae kutokana na kuwa na wachezaji wengi ambao wanacheza eneo hilo la kiungo mshambuliaji. Ross ametambulishwa leo katika klabu ya Nice inayoshiriki Ligue 1 huko Paris.

Nice ambayo sasa imesajili wachezaji na wengine wakiwa kwa mkopo pale kama vile golikipa Schmeichel, kutoka Leicester City, Malang Sarr beki huyo akitokea The Blues, na Barkley ambae pia katoka Chelsea.
Timu hiyo bado haijakaa sawa kwani mpaka sasa ndani ya mechi sita imeshinda mechi 1, sare mbili na imepoteza mechi tatu ambayo ya sita ni ya jana aliyopoteza dhidi ya Monaco akiwa nyumbani kwake. Huku kwenye msimamo wa Ligue 1 ikishikilia nafasi ya 16.

