Mchezaji wa klabu ya Manchester City Bernado Silva ambaye ana umri wa miaka 28 na anacheza anacheza nafasi ya kiungo katika timu yake hiyo baba yake mzazi amesema kuwa si wakati sahihi wa yeye kuondoka klabuni hapo.

Kuondoka kwa Bernado Silva City hakujatimia kwani haukuwa wakati mwafaka wa yeye kutimka klabuni hapo ambapo ada ofa yake ilichelewa alisema hayo baba yake Paulo. Mchezaji huyu wa Kireno alihusishwa vikali kuondoka katika viwanja hivyo vya Etihad kkatika dirisha hili la msimu wa joto huku klabu ya Barcelona wakionekana kuwa namba moja kuvutiwa nae.
Lakini hatimaye mchezaji huyo aliamua kubaki na mabingwa watetezi mfululizo wa EPL na kufichua baadae kuwa ombi la kuchelewa lilifika kwa mwombaji ambaye jina lake halikutajwa kufika.

Silva alipendekeza kuwa kutokuwa na uwezo wa City kutosajili mbadala wake mwishoni mwa dirisha hili, kulisitisha uhamisho huo, na baba yake aliongezea kwa kusema kuwa uhamisho huo haukufanya kazi kwa kila mtu kwa wakati huo.
“Kulikuwa na mazungumzo mengi lakini si ofa halisi kwa wakati ambao tulidhani inaweza kutolewa”. Alisema Paulo.
Bernado Silva mpaka sasa katika ligi kuu ya Uingereza ana mabao mawili na assist mbili ambapo ameiwezesha timu yake kucheza michezo sita mpaka sasa bila kupoteza hata mchezo mmoja.

