Yakiwa ni masaa machache yamebaki kabla ya kufugwa kwa dirisha kubwa la usajili Ulaya, mchezaji wa timu ya Taifa ya Ureno na klabu ya Manchester City Bernado Silva amesema kuwa hataondoka klabuni hapo kwa hajapokea ofa yoyote na mustakabali wake upo City.
“Ninabaki Manchester, Hapa nina furaha na uamuzi umefanywa” aliiambia @polballus
Mwanzo, tetesi zilikuwa zikimuhusisha na kujiunga na Barcelona lakini taarifa zilizotoka ni kuwa ataendelea kuitumikia Manchester City msimu huu ambao wapo kwenye kiwango bora sana.

Bernado ambaye anacheza kwenye nafasi ya kiungo amekuwa na mchango mkubwa sana pale Etihad kwani licha ya kuwa kiungo mshambuliaji ana uwezo mkubwa pia wa kupachika mabao, anajituma sana kitu ambacho kimeleta mafanikio chanya klabuni hapo.


