Sergino Dest amejiunga na klabu ya Ac Milan nchini Italia akitokea klabu ya Fc Barcelona kwa mkopo wa msimu mzima.
Dest anakwenda kwa wababe hao wa Italia kwa mkopo wa msimu mzima huku kukiwa na chaguo la kununuliwa jumla kwa kiasi cha €milioni 10 na mkataba mnono wa miaka minne kama Ac Milan watavutiwa kutoa kiasi hicho cha pesa baada ya mkopo wake kumalizika.

Klabu ya Fc Barcelona imemuachia beki huyo raia wa marekani baada ya kua na uhakika wa safu ya ulinzi nzuri baada ya kuongeza wachezaji kwenye eneo hilo ambao wanaweza kucheza kwa kiwango bora kabisa.
Beki huyo wa zamani wa Ajax ya uholanzi amekua hana wakati mzuri sana tangu kutua klabuni hapo misimu kadhaa nyuma huku akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara kitu kilichofanya nafasi yake pia kua finyu kikosini na kutimkia klabu ya Ac Milan.

