Bernado Silva amekuwa nguzo kubwa sana ndani ya kikosi cha Guardiola msimu huu akionesha uwezo wa juu kabisa ndani ya ligi hiyo upande wa kufunga, kutoa pasi za muhimu na hata kuisaidia kwa namna nyingi timu yake kupata matokeo yanayoridhisha. Ikumbukwe, City kwa sasa ndiyo wanaoongoza ligi hiyo wakiwapunguza kasi Liverpool waliokuwa wanaifukuzia nafasi hiyo ya kwanza.
Mchezaji huyo amesaini kandarasi itakayofanya aendelee kusalia katika kikosi cha matajiri hao hadi 2025, ikiwa ni hatua kubwa na mafanikio makubwa kwa raia huyo wa Ureno ambaye uchezaji wake umekuwa ukiimarika siku hadi siku ndani ya kikosi hicho chenye kiu kubwa ya vikombe.
Silva alijiunga na Manchester City kwa uhamisho wa £43.5m baada ya kuonesha uwezo wa kustaajabisha alipokuwa mchezaji wa Monaco baada ya kutwaa ubingwa wa ndani ya ligi ya Ufaransa na baadaye kukiondoa kikosi kilichokuwa chini ya Guardiola kwa kipindi kile katika michuano ya klabu bingwa.
Mkataba wa awali wa raia huyo wa Ureno unaisha 2022 lakini amefikiriwa mapema sana na wamiliki wa timu hiyo kwa kuamini anachokifanya ndani ya klabu hiyo. Pamoja na kuwa mkataba wake ulikuwa bado mbichi kabisa lakini amekuwa mchezaji aliyepewa matumaini ya awali kuendelea kuwa chini ya utawala wa timu hiyo.
Silva alipoulizwa juu ya furaha ya namna gani anayo baada ya kuongezewa miaka mitatu ya mkataba ndani ya timu hiyo alisema ana furaha kubwa sana kuendelea kusalia katika kikosi ambacho ni bora zaidi, mwalimu bora, wachezaji wenye uwezo wa pekee, mashabiki wenye upendo na klabu inayothamini nafasi ya kila mchezaji kwa kumpa kila kinachoonekana bora.
Ameweza kuwachezea City jumla ya mechi 53 akiwa tayari ameshinda kombe la ligi kuu na lile la EFL 2017/18 lakini katika misimu yake yote msimu huu unaonekana ni wa pekee sana kwake kutokana na kufanya makubwa ambayo yamekuwa magumu sana mbele ya timu nyingi za upinzani anazokutana nazo.
Anaonekana kuwa mbadala wa De Bruyne ambaye kwa msimu huu amekuwa akikumbana na majeraha ya mara kwa mara yanayomuweka nje ya uwanja katika raundi nyingi anapokuwa kwenye shughuli za kuitafutia matokeo ambayo yangeweza kusaidia kikosi hicho kikaendelea kuwa bora zaidi ya ilivyo sasa na kupata matokeo zaidi.
Aliweza kufunga pia katika mechi yao ya kampeni kuelekea robo fainali ambapo waliweza kuwapa dozi ya wiki nzima 7-0 na kufanya matokeo kuwa 10-2. Baadhi ya wachezaji wanaoungana na Silva kusaini kikataba mipya ni De Bruyne, Ederson, Sterling, Laporte na Gabriel Jesus. Kwake Ikay amekuta wanashindwa kufikia makubaliano ya mkataba mpya.


Povel tz
Habar njema
Shakila mrope
🔥🔥🔥🔥🔥