Liverpool wamefanikiwa kumuadhibu Bayern katika mchezo wao wa klabu bingwa Ulaya pale walipokutana na mpinzani wao huko Ujerumani. Liverpool walionekana kama kuzembea kutafuta magoli lakini wakiwaruhusu Bayern wacheze mpira watakavyo wao ila wao walitumia mbinu ya mashambulizi ya kushtukiza yaliyowapa matunda.
Mechi ilitawaliwa na ufundi wa kutosha ambapo kila timu ilikuwa ikijitahidi kupata matokeo ya mapema ili kujilinda maana kila mechi ina ugumu wake ambao kupata matokeo ya haraka yangesaidia sana kuwapa matumaini ya kusonga mbele zaidi. Kumalizika kwa 0-0 katika mechi ya awali kulimpa nafasi Liverpool ambaye alikuwa hajaruhusu goli lolote nyumbani.
Baada ya kutafutana sana katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo, timu hizo zilionekana kushambuliana mara kwa mara kwa kuviziana pale mmoja anapofanya makosa anaadhibiwa kwa alichokisababisha. Kama siku zote ilivyo kwamba soka ni mchezo wa makosa na inapotokea hivyo timu husika inatumia nafasi kuongoza.

Haikuchukua kitambo sana pale Sadio Mane aliposuka mipango yake na kuifungia Liverpool goli ambalo liliamsha kasi ya mchezo uliokuwa umeonekana kupoa kutokana na timu zote mbili kucheza mchezo wa tahadhari. Baada ya goli hilo sasa likashuhudiwa soka safi lenye ushindani, ambapo bado waliendelea kutafuta kitu kimoja tu basi.
Baada ya mechi kuchangamka na Bayern kuanza kutafuta mbinu ya kurudi mchezoni na kuwafanya Liverpool wasiendelee kupandisha sana mashambulizi walijitahidi kutawala eneo la katikati la uwanja; kitu kilichowafanya wapate goli la kufutia machozi kupitia kwa Matip ambaye alijifunga katika harakati za kuokoa mpira uliokuwa karibu kuingia nyavuni.
Matokeo yaliendelea kusomeka 1-1 kabla Van Dijk hajawapa haki yao Bayern baada ya kufanya makosa ya kushindwa kumzuia aliporuka kichwa huru na kufunga goli la pili ambalo liliongeza machungu mazito kwa wenyeji hao waliokuwa na mategemeo makubwa mno kupata matokeo mazuri wakiwa nyumbani na kufanya Liverpool kuwa kifua mbele kwa 2-1.
Kama haitoshi tena Mane alirudi nyavuni baada ya kupokea mpira mzuri kutoka kwa Salah uliomfanya apigilie msumari mwingine kwa kichwa safi sana kilichomshinda mlinda mlango Nuer ambaye hakuwa kwenye ubora wake wa mara zote akiwa uwanjani na klabu hiyo.
Kutokana na matokeo hayo sasa, Liverpool anaungana na Waingereza wenzake wakiwemo Manchester United, Manchester City, Tottenham na wengine kama Barcelona, Ajax, Juventus, Porto katika hatua ya robo fainali kitu ambacho kinahitaji umakini zaidi ya ilivyo sasa baada ya mechi hizo kuisha hatua hiyo ya 16 bora. Hatua hiyo mara nyingi huwa ni ngumu sana maana hakuna timu ambayo hucheza chini ya kiwango inaposogea katika hatua hiyo. Kinachotegemewa ndani yake huwa ni soka safi lenye ufundi mwingi sana.


Povel
Habar njema