Arsenal Yachinja Ikirudi Kileleni Epl

Klabu ya Arsenal imeweza kupata ushindi mnono dhidi ya klabu ya Nottingham Forest katika mchezo wa ligi kuu Uingereza, Washika mitutu wa London wamefanikiwa kushinda magoli matano kwa bila wakiwa katika dimba lao la nyumbani.

Klabu hiyo imepata ushindi huo huku ikicheza kwa mamlaka makubwa na kiwango cha juu katika mchezo huo, klabu hiyo ilipata magoli yake kupitia kwa Gabriel Martinelli,Reiss Nelson aliefunga magoli mawili, Thomas Partey, na nahodha wa klabu hiyo Martin Odeergard akikamilisha karamu ya magoli.arsenalArsenal baada ya ushindi mnono wa leo wanarejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakifikisha alama 31 katika michezo 12 waliyocheza huku wakiwashusha klabu ya Manchester City wenye alama 29 katika nafasi ya pili.

Vijana wa Mikel Arteta msimu wamekua kwenye kiwango bora sana kwani mpaka sasa wamepoteza michezo miwili tu katika mashindano yote waliyoshiriki msimu huu.arsenalLakini hofu imezuka ndani ya klabu ya Arsenal  baada ya nyota wa klabu hiyo Bukayo Saka kuumia na kutolewa ndani ya kipindi cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Riess Nelson.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.