Yanga Yaifuata Namungo Ruangwa

Baada ya ushindi wa jana klabu ya Yanga imeifuata Namungo huko Lindi kwaajili ya mchezo wao unaofuata wa Ligi kuu ya NBC unaotarajiwa kupigwa siku ya Jumatano tarehe 7.

 

Yanga Yaifuata Namungo Ruangwa

Kikosi hicho kimewasili Mtwara na kitapumzika na kufanya mazoezi jioni ya leo kabla ya kuanza safari ya kwenda Ruangwa kesho, huku mshambuliaji wao Fiston Mayele akiambatana na kikosi hicho cha Yanga.

Mayele aliukosa mchezo wa jana dhidi ya Tanzania Prisons ambapo walishinda kwa bao moja kwa bila katika dakika ya 90 ya mchezo kupitia kwa kiungo wao Feisal Salum na kufanya wapae kileleni kwenye msimamo wa Ligi.

Yanga Yaifuata Namungo Ruangwa

Tangu Namungo apande ligi mwaka 2019 Yanga amepata ushindi mara moja tuu, huku timu hiyo ikionekana kuleta ushindani mbele ya mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.