Kiungo wa Yanga Khalid Aucho amaeomba kuondoka klabuni hapo na kufanya kuiweka klabu hiyo katika wakati mgumu baada ya uamuzi huo huku pia wachezaji wengine mikataba yao ikitarajia kumalizika.

Timu hiyo inahesabu masaa kabla ya kushuka Dimbani kwa Mkapa kumenyana na Tanzania Prisons katika mechi ya Ligi Kuu baada ya kutoka kupoteza mechi yao iliyopita dhidi ya Ihefu.
Lakini pia kiungo wao kutoka Zanzibar Feisal Salum mkataba wake unalaizika hivi karibuni na viongozi wa timu hiyo wanataka kumpa mkataba mpya huku ofa mbalimbali zikimiminika ikiwemo ya Azam FC.
Aucho yeye ameomba asiongezwe mkataba mkataba mpya ili aweze kuondoka Jangwani hapo na kwenda kujiunga na timu huko Uarabuni, huku mkataba wake ukielekea kumalizika .

Pia taarifa zingine zinasema kuwa beki wa kati Dickon Job na golikipa wao namba moja Djigui Diarra, viongozi wanafanya harakati za kuzungumza nao ili wawaongezee mkataba kabla ya ile ya awali haijaisha.

