KIUNGO nyota wa Klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Uganda “The Cranes” Khalid Aucho yupo mbioni kutimka mitaa ya Twiga na Jangwani baada ya kugoma kusaini mkataba mpya.
Taarifa zilizothibitishwa na chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Yanga zimebainisha kuwa Aucho amegoma kusaini mkataba mpya kwa sababu amepata ofa nono kutoka klabu moja inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Saudi Arabia.
Ikumbukwe mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu na tayari mabosi wa timu yake wameendeleza jtihada zao za kumshawishi nyota huyo kubakia Jangwani.
Akiwa na Yanga, ameisaidia timu hiyo kupata ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa mara ya 28 baada ya kumaliza utawala wa Simba SC uliodumu kwa zaidi ya misimu minne mfululizo.