Tottenham Yaendelea Kupitia Kipindi Kigumu

Klabu ya Tottenham Hotspurs imeendelea kupitia wakati mgumu katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kua na mfululizo mbaya wa matokeo katika siku za hivi karibuni.

Tottenham jana walikumbana na kipigo cha pili mfululizo katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kuruhusu kufungwa na klabu ya Manchester City kwa mabao manne kwa mawili. Hii inaendelea kuwaeka klabu hiyo kwenye mazingira magumu kwenye mbio za kuwania nafasi nne za juu.tottenhamVijana wa Antonio Conte walianza vizuri mchezo wa jana baada ya kuongoza kwa mabao mawili kwa bila katika kipindi cha kwanza katika mchezo huo, Mabao ya Dejan Klushevski na Emerson Royal yalitosha kuipa Spurs uongozi katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Klabu ya Tottenham ilikutana na kadhia kubwa kipindi cha pili katika mchezo wa jana baada ya meza kupinduliwa kibabe na klabu ya Manchester City, Baada ya mabao yote kusawazishwa na kuongezwa mabao mengine mawili na mchezo kumalizika wakifungwa mabao manne kwa mawili.tottenhamTottenham Hotspurs wamecheza michezo mitano ya ligi kuu ya Uingereza baada ya michuano ya kombe la dunia ikiwa imefanikiwa kushinda mchezo mmoja pekee huku ikipoteza mitatu na kusare mchezo mmoja. Kupitia kiwango kinachooneshwa na klabu hiyo ni wazi itapata wakati mgumu kuingia kwenye nafasi nne za juu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.