Tottenham walionyesha kushtushwa na tukio lililomshuhudia mlinda mlango wa Arsenal Aaron Ramsdale akishambuliwa na shabiki mwishoni mwa mchezo wa jana wa dabi ya London kaskazini.

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Hotspur ulikuwa umemalizika tu wakati Ramsdale akiwa karibu na eneo lenye mashabiki wa nyumbani, alilengwa na shabiki mmoja ambaye alipanda kwenye uzio wa uwanja na kumshambulia.
Huenda kukawa na madhara makubwa kwa Tottenham, baada ya hatua za kiusalama kushindwa kumzuia shabiki huyo kuwa karibu sana na mchezaji huyo wa Kimataifa wa Uingereza.
Kwa sasa, Spurs wamesema wamedhamiria kumtambua mwanamume huyo, ambaye alikimbia kupitia stendi baada ya tukio hilo lililonaswa na kamera za televisheni.

Tottenham walisema katika taarifa: “Tunashangazwa na tabia ya shabiki aliyejaribu kumshambulia kipa wa Arsenal Aaron Ramsdale mwishoni mwa mechi ya leo. Vurugu za aina yoyote hazina nafasi katika soka.”
Klabu imekagua picha zake za CCTV ili kumtambua mwanaume huyo na itashirikiana na Polisi wa Met, Arsenal na Aaron Ramsdale kuchukua hatua kali zaidi, ikiwa ni pamoja na kupigwa marufuku mara moja kutoka Tottenham Hotspur Stadium.
Shirikisho la Kitaifa la Uingereza, Chama cha Soka, lilisema tukio hilo halikubaliki kabisa na likasema litachukua sehemu kamili katika uchunguzi.

Ilitoa taarifa iliyosomeka: “Tunalaani vikali tukio lililohusisha mtazamaji aliyefuatia mchuano wa leo wa Ligi Kuu kati ya Spur na Arsenal.”
Hii ni tabia isiyokubalika kabisa na tutashirikiana na polisi, mamlaka husika na vilabu kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa. Alimaliza hivyo.

