Tottenham Dhidi ya Arsenal Moto Kuwaka London Derby

Klabu ya Tottenham Hotspurs itawakaribisha mahasimu zao kutoka jiji la London klabu ya Arsenal katika mchezo ligi kuu ya Uingereza ambao pia utakua ni derby ya London kaskazini.

Klabu ya Tottenham itakua na kibarua kizito dhidi ya vinara wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya soka ya Arsenal, Mchezo huo unatarajiwa kua na upinzani mkubwa kutokana na asili ya mchezo wenyewe ambao ni derby lakini pia ubora wa vikosi vyote viwili.tottenhamVijana wa Antonio Conte wanahitaji kupata matokeo ya alama tatu dhidi ya klabu ya Arsenal katika mchezo wa leo ili kuweza kujiwekea mazingira mazuri ya kugombea nafasi nne za juu. Kwani tangu kurejea kwa ligi kuu ya Uingereza klabu hiyo imeshinda mchezo mmoja kati ya mitatu ambayo imecheza.

Klabu ya soka ya Arsenal wao wako kwenye ubora mkubwa mpaka sasa wakiwa wanaongoza ligi kuu ya Uingereza, Klabu ya Arsenal wao wameshinda michezo yao minne waliyocheza ya ligi kuu tangu michuano ya kombe la dunia imalizike.tottenhamKlabu ya Tottenham inaenda kwenye mchezo wa leo dhidi ya Arsenal ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa jumla ya mabao matatu kwa moja, Huku Arsenal wao wakiwa hawahitaji kupoteza mchezo huo ili kujiimarisha kwenye mbio za ubingwa msimu huu.

Acha ujumbe