Ripoti zinadai kuwa Tottenham Hotspur wanafikiria kuwasilisha ofa Januari kwa nyota wa Roma, Nicolò Zaniolo kwani vilabu vingine vya Italia vitatoa ofa tu msimu wa joto.

Hali ya Zaniolo kwenye Uwanja wa Stadio Olimpico inazidi kuwa ya wasiwasi baada ya kukejeliwa waziwazi na baadhi ya mashabiki wakati wa ushindi wa 1-0 wa Coppa Italia dhidi ya Genoa.
Uchezaji wake wa hivi majuzi na mtazamo wake wa jumla umeudhi uongozi wa klabu hiyo na kwa kuwa mkataba wake unatarajiwa kumalizika Juni 2024, hakuna maendeleo ya kujadili mkataba mpya.

Kulingana na mtaalam wa uhamisho wa Sportitalia na Gazzetta dello Sport Alfredo Pedullà, Tottenham ya Antonio Conte inafikiria kuhusu uhamisho wa Januari kwa mchezaji huyo wa Kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 23.
West Ham United na Nottingham Forrest ukiacha Tottenham pia wanafuatilia hali hiyo, huku mkataba wake ukidorora, bei pia inashuka kutoka €50m hadi €30m na kumekuwa na nia kutoka kwa timu za Serie A kama vile Juventus, Napoli na Milan, lakini watakuwa katika hali ya kufanya pendekezo mwishoni mwa msimu.

Zaniolo aliona kazi yake kukwama kutokana na majeraha mawili mabaya ya goti, lakini akafunga bao la ushindi katika Fainali ya Ligi ya Europa msimu uliopita.
Mpaka sasa msimu huu ana mabao mawili na asisti tatu katika mechi 17 za kimashindano akiwa na Roma.

