Ten Hag Aahidi Maboresho Zaidi Man United

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag ameahidi maboresho zaidi ndani ya klabu hiyo baada ya timu hiyo kuanza kuonekana imekaa kwenye kiwango kizuri.

Klabu ya Manchester United ambayo imekua ikipitia kipindi kigumu kwa muda mrefu sasa na kushindwa kubeba taji lolote kwa takribani kipindi cha miaka sita sasa, Lakini klabu hiyo inaonekana kuanza kuimarika chini ya kocha Erik Ten Hag.ten hagKocha huyo anasema anataka kurudisha utamaduni wa ushindi ndani ya klabu hiyo kama ambavyo ilikua imezoelekea hapo awali kipindi cha kocha Sir Alex Ferguson, Klabu ya Manchester United imepoteza sifa na ubora wake kwa miaka ya hivi karibuni kitu ambacho kocha huyo anataka kukirudisha ndani ya klabu hiyo.

Kocha Erik Ten Hag aliulizwa na wanahabari juu ya Man United kuimarika zaidi na yeye alikiri kwa kusemka ana imani maboresho yataendelea kuwepo na kwakua kwasasa wako kwenye muelekeo sahihi basi anaamini timu hiyo itafika kwenye kiwango amabcho inapaswa kuwepo.ten hagKocha huyo pia amesema kama unataka kushindana katika nafasi za juu katika siku zijazo basi unapaswa kujiimarisha zaidi na ndio kitu anachofanyia kazi ndani ya timu hiyo. Klabu ya Manchester United itakwenda kumenyana na vinara wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Arsenal katika dimba la Emirates leo mchezo unaotarajiwa kua mkali na wenye mvuto zaidi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.