Bielsa Aongoza Kinyang'anyiro cha Ukocha Everton

Kocha wa zamani wa vilabu vya Leeds United na Athletic Bilbao Marcelo Bielsa anaongoza kinyang’anyiro cha makocha wanaotajwa kuwania kibarua cha ukocha ndani ya klabu ya Everton.

Klabu ya Everton ilifanikiwa kumfukuza kocha wake ambaye ni gwiji wa zamani wa klabu ya Chelsea Frank Lampard siku mbili zilizopita, Hii imefanya kuanza kutafuta kocha ambaye atavaa viatu vya gwiji huyo ambaye ameiacha klabu hiyo kwenye hali mbaya kunako ligi kuu ya Uingereza.bielsaTaarifa zinaeleza makocha mbalimbali wanatajwa kuwania kibarua cha klabu hiyo ni kocha wa zamani wa Burnley Sean Dyche, Ralf Hansenhuttl, na kocha mkongwe Marcelo Bielsa ambaye ndio inatajwa kama anaiongoza orodha hiyo na ndio mwenye nafasi kubwa ya kupewa nafasi ya kua kocha mkuu wa klabu ya Everton.

Klabu ya Everton ipo kwenye kipindi kigumu zaidi kwenye ligi kuu ya Uingereza kwani mpaka wanafikia kumtimua kazi aliyekua kocha wa klabu hiyo Frank Lampard walikua wanashika nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama 15 wakiwa wamecheza michezo 20.bielsaMarcelo Bielsa ni mwalimu ambaye ana sifa kubwa barani ulaya kutoakana na uwezo wake katika kufundisha soka haswa mpira mzuri wenye kasi zaidi, Huku akiwa ni historoa nzuri kwenye vilabu mbalimbali kama Leeds United ya Uingereza akifanikiwa kuipandisha ligi kuu ya Uingereza pamoja na Athletic Bilbao ya nchini Hispania. Na ndio kocha ambaye yupo kwenye nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya Lampard ndani ya klabu ya Everton.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.