Rashford Achaguliwa Kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Epl

Mshambuliaji anayefanya vizuri ndani ya klabu ya Manchester United Marcus Rashford amechaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza ndani ya mwezi Januari.

Mchezaji huyo anawania tuzo hiyo pamoja na wachezaji wengine kama Harry Kane kutoka Tottenham Hotspurs, Bukayo Saka kutoka Arsenal na Mitoma kutoka Brighton Hove and Albion ndio wachezaji watakaungana na Marcus Rashford kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Januari ndani ya ligi kuu ya Uingereza.RashfordMarcus Rashford pamoja na Bukayo Saka wanawania tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo kwani waliwania pamoja tuzo ya mwezi November na Disemba ambazo zilijumuishwa pamoja na Bukaya Saka akifanikiwa kushinda tuzo hiyo na sasa wamefanikiwa kukutana tena kwenye kinyang’anyiro hicho.

Staa huyo wa Man United amekua na ubora mkubwa sana tangu arudi kutoka kwenye michuano ya kombe la dunia na kufanikiw akufunga mabao kumi mpaka sasa, Hii inamfanya kua mchezaji aliefunga mabao mengi kwenye ligi kubwa tano barani ulaya.RashfordMarcus Rashford binafsi anaingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania mchezaji bora wa mwezi ligi kuu ya Uingereza kwa mara ya tatu msimu huu huku akifanikiwa kushinda mara moja, Hii inaonesha kwa namna gani mchezaji huyo ameimarisha uwezo wake ndani ya msimu huu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.