Rashford Aendelea Kuuwasha Moto

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Uingereza Marcus Rashford ameendeleza moto wake ambao ameuwasha katika michezo ya hivi karibuni.

Marcus Rashford amefunga mabao nane kwenye michezo saba ambayo klabu ya Manchester United imecheza baada ya michuano ya kombe la dunia, Leo katika mchezo dhidi ya Manchester City mchezaji huyo amefunga bao lake la nane na kuendeleza moto wake ambao haujapata wakuuzima mpaka sasa.RashfordMshambuliaji huyo ambaye alikua ana msimu mbaya sana msimu uliomalizika lakini ndani ya msimu huu ni kama amezaliwa upya kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha, Hii ni kutokana na idadi ya mabao ambao aliyafunga msimu uliomalizika na sasa kua tofauti kabisa.

Marcus Rashford pia amefanikiwa kuweka rekodi nyingi ya kufunga katika michezo tisa mfululizo ambayo klabu yake ya Manchester United imecheza nyumbani katika dimba la Old Trafford. Mchezaji huyo anakua ndio mchezaji mwenye mabao mengi na kiwango bora zaidi tangu kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia.RashfordMshambuliaji huyo ameimarika sana kwenye kikosi cha Manchester United chini ya kocha Erik Teb Hag na kuibuka kua msaada mkubwa sana ndani ya klabu hiyo, Pia mwalimu mpya wa washambuliaji klabuni hapo Benni Mccarthy inaelzwa amefanya kazi kubwa kurudisha ubora wa Marcus Rashford.

Acha ujumbe