Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba Salim Try again amewaahidi makubwa mashabiki wa klabu ya Simba kuelekea mwisho wa dirisha dogo la usajili.
Salim Try again amewataka mashabiki wa Simba kutulia kuelekea mwishoni mwa dirisha dogo la Januari ambapo klabu ya Simba imesajili mchezaji mmoja mpaka wakati huu, Mashabiki wa klabu hiyo wanatarajia usajili mkubwa ndani ya klabu yao baada ya kuanza kwa kusuasua ndani ya msimu huu.
Kupitia mitandao yake ya kijamii mwenyekiti huyo ameandika “Anaefurahi mwisho ndio anafurahi zaidi, na anafurahi kwelikweli” akimaanisha kua kuelekea mwishoni mwa dirisha hili klabu hiyo inatarajia kufanya usajili mkubwa ambao utawafurahisha mashabiki wa klabu ya soka ya Simba.
Salim Try again alisema kua kwenye dirisha la dogo la mwezi Januari klabu ya soka ya Simba itafanya usajili mkubwa na mzuri wa kuimarisha kikosi chao, Hivo kupitia kauli hiyo ameonesha kuwakumbusha mashabiki wa klabu hiyo waondoe wasiwasi kua anafanyia kazi ahadi ambayo aliitoa mapema kabla ya dirisha kufunguliwa.
Klabu ya soka ya Simba imetoa taarifa kua leo usiku itatambulisha mchezaji wake mpya na hii moja kwa moja inaonesha kua kauli ambayo aliitoa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Salim Try again ni ya uhakika na klabu hiyo itafanya usajili mzuri ndani ya dirisha hili, Ambapo mashabiki wa klabu hiyo waliingia hofu kwani siku zinamalizika na hawaoni usajili ukifanyika.

