Kocha wa klabu ya PSG amethibitisha kua staa wa klabu hiyo Lionel Messi atakosekana katika mchezo wa ligi kuu ya Ufaransa wikiendi hii dhidi ya Monaco kutokana na majeraha.
Staa Lionel Messi ambaye alishiriki mchezo wa kombe la Ufaransa katikati ya wiki hii dhidi ya klabu ya Olympique Marseille na klabu ya PSG kutupwa nje ya michuano, Kocha Galtier amesema staa huyo atakosekana katika mchezo dhidi ya Monaco.
Staa huyo alipata maumivu ya misuli katika mchezo dhidi ya Marseille kitu ambacho kimeleta wasiwasi kwa staa huyo kukosekana katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Bayern Munich siku ya jumanne, Lakini kocha Galtier amesema nyota huyo atarejea mazoezini siku ya jumatatu.
Kocha Galtier aeweka wazi kua kumkosa Messi katika mchezo dhidi ya Monaco ni pengo kwa upande wao kutokana na umuhimu ambao amekua nao nyota huyo kikosini, Lakini kutokana na majeraha ambayo ameyapata staa huyo ni wazi itampasa akosekane katika mchezo dhidi ya Monaco.
Lionel Messi ataungana na staa mwingine ndani ya klabu hiyo Kylian Mbappe ambaye alipata majeraha wiki kadhaa zilizopita, Lakini mshindi huyo wa kombe la dunia ana asilimia kubwa za kuwepo katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Bayern Munich tofauti na Mbappe ambae atakosekana katika mchezo huo.

