Real Madrid Kulisaka Taji la Tano Klabu Bingwa ya Dunia

Klabu ya Real Madrid leo itashuka dimbani kumenyana na klabu ya Al-Hilal katika fainali ya klabu bingwa ya dunia kulitafuta taji lao la tano la klabu bingwa ya dunia.

Real Madrid ilifanikiw akushinda mchezo wake wa nusu fainali wa klabu bingwa ya dunia dhidi ya klabu ya Al- Ahly ya nchini Misri kwa jumla ya mabao manne kwa moja, Hivo klabu hiyo itakua inawinda taji lake la tano katika michuano hiyo inayopigwa nchini Morocco.Real MadridMabingwa hao watetezi wa ulaya wamewahi kushinda taji hilo mara nne tayari ndani ya miaka ya 2014,2016,2017, na mwaka 2018 na kua kinara katika taji hilo kama mabavyo ni vinara katika taji la ligi ya mabingwa ulaya wakishinda taji hilo mara 14.

Klabu ya Real Madrid pia itakua kwenye wakati mzuri kwani itawapokea wachezaji wake muhimu wawili kwenye kikosi chao, Ambao ni mshambuliaji matata wa klabu hiyo Karim Benzema pamoja na beki wao wa kutumainiwa klabuni hapo Eder Millitao.Real MadridReal Madrid kama watafanikiwa kushinda taji la leo la klabu bingwa ya dunia basi watafanikiw kuweka rekodi ya kua timu ya kwanza kufikisha mataji matano ya klabu bingwa ya dunia, Hii itaendelea kuonesha ukubwa wa klabu hiyo kwani kwenye mataji yote makubwa klabu hiyo imekua ikiwa kinara.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.