Klabu ya soka ya Simba itakua klabu pekee kutoka Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki kushiriki michuano mikubwa ya soka barani Afrika ambayo inatarjiwa kuanza mwaka huu inayojulikana kama Super League.
Michuano ya Super League ni michuano ambayo ipo chini ya shirikisho la mpira barani Afrika CAF na wazo la kwanza la michuano hii lilitoka kwa Rais wa shirikisho la soka duniani Gianni Infantino mwaka 2019, Na michuano hiyo kupitishwa rasmi mwaka 2022 mwezi Agosti.
Klabu ya Simba wao wanakua wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano hiyo ambayo itakua inaingiza kipato kikubwa zaidi kwa vilabu ambavyo vitakua vinashiriki, Kwani kila klabu ambayo itashiriki michuano hiyo itapata kiasi cha shilingi bilioni tano na bingw atapokea kiasi cha shilingi bilioni 27 kwa pesa za kitanzania.
Mipango ya kuanzisha michuano hii ni kuingiza kipato kikubwa zaidi kwa vilabu na miongoni mwa vilabu ambavyo vitakua vinashiriki michuano hii lazima viwe na nguvu ya kiuchumi, Lakini pia iwe ni miongoni mwa klabu ambayo inafanya vizuri katika michuano ya CAF.
Klabu ya Simba itaungana na vilabu kama Al Ahly, Mamelodi Sundowns,Petro Luanda, Tp Mazembe, Horoya, Esperance de Tunis, pamoja na Wydad Casablanca katika michuano ya Super League ambayo inatarjwa kutimua vumbi kuanzia mwaka huu mwezi Agosti ikiwa ni msimu wa kwanza wa michuano hiyo.

