Klabu ya Chelsea bado imeendelea kuchechemea kunako ligi kuu ya Uingereza baada ya kukubali kichapo cha bao moja kwa bila dhidi ya klabu ya Southampton katika dimba lao la nyumbani la Stamford Bridge.
Klabu ya Chelsea imebakubali kichapo cha bao moja kwa bila dhidi ya klabu ya Southampton ambao wanashika mkia kunako ligi kuu ya Uingereza, Bao la mkwaju wa faulo kupitia kiungo wa klabu ya Southampton James Ward Prowse dakika ya 45 ya mchezo na kupeleka kilio darajani.
Southampton wao baada ya kushinda mchezo wa leo wanafanikiwa kufikisha alama 18 na unakua mchezo wao wa tano kushinda msimu huu kati ya michezo 23, Baada ya mchezo huu inaweza kua nafasi kwa klabu hiyo kujitengeneza na kutoka mkiani ambapo wapo kwasasa.
Klabu ya Chelsea baada ya kupokea kichapo katika mchezo wa leo klabu hiyo imefikisha mchezo wa sita wa ligi kuu ya Uingereza na kufanikiwa kupata ushindi katika mchezo mmoja pekee, Kupitia hali inayoendelea ndani ya klabu hiyo ni wazi kua kocha Graham Potter ana wakati mgumu sana kutokana na usajili uliofanyika klabuni hapo.
Chelsea wanaendela kusalia nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama zao 31 baada ya kucheza michezo 23 mpaka wakati huu, Klabu hiyo itakua na wakati mgumu sana kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya.

