Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Antonio Conte amesema kua hatma yake na klabu hiyo itajulikana baada ya msimu huu kumalizika kwakua watakaa mezani na klabu hiyo.
Antonio Conte amekua akizungumzwa huenda akachana na klabu ya Tottenham au kufukuzwa klabuni hapo kutokana na mwenendo wa klabu hiyo mpaka sasa, Spurs wamekua hawana muendelezo wa matokokeo katika michezo yao mbalimbali ambayo wamekua wakicheza.
Tottenham mpaka sasa hawana taji lolote ambalo wanaonekana wanaweza kubeba kwani ligi kuu ya Uingereza wanagombea ushiriki wa michuano ya ulaya msimu ujao, Fa pna Carabao Cup tayari wameshatolewa huku ligi ya mabingwa ulaya wakitupwa nje jana na klabu ya Ac Milan katika dimba lao la nyumbani.
Taarifa zinaeleza kua endapo kocha Antonio Conte atashindwa kumaliza kwenye nafasi nne za juu msimu huu, Huenda klabu hiyo ikaachana na kocha huyo raia wa kimataidfa wa Italia baada ya kushindwa kuivusha timu hiyo kucheza ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao.
Kocha Conte alifanikiwa kuiwezesha klabu ya Tottenham kucheza michuano ya ligi ya mabingwa ulaya, Lakini msimu huu inaonekana mambo kua tofauti ndani ya klabu hiyo kwani muendendo klabu ya Tottenham mpaka sasa haujaeleweka kwani wamekua wakipata matokeo kwa kusuasua.

