Conte Kurejea Tottenham Wiki Ijayo

Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Antonio Conte atarejea kwenye majukumu yake ndani ya klabu hiyo wiki ijayo mazungumzo hayo ameyatoa kocha wa muda klabuni hapo Cristian Stellini.

Kocha Conte alifanyiwa upasuaji wa kibofu mwanzoni mwa mwezi Febuari baada ya kusikia maumivu makali ya tumbo kwa wakati huu yupo nchini kwao Italia akiendelea kujiuguza, Lakini kwa mujibu wa kocha Stellini kocha huyo atarejea klabuni hapo wiki ijayo.ConteKlabu ya Tottenham imefanikiwa kushinda michezo yake miwili ya ligi kuu bila ya kuwepo kwa kocha wake mkuu, Huku ikisimamiwa na kocha Cristian Stellini ambaye ameiongoza klabu hiyo kushinda michezo miwili mfululizo ya ligi kuu ya Uingereza ukiwemo wa leo dhidi ya Chelsea.

Kocha Antonio Conte ameukosa mchezo muhimu kwa klabu yake Tottenham ikifanikiwa kuisambaratisha klabu ya Chelsea kwa mabao mawili kwa bila na kufuta uteja ambao wamekua nao kwa muda sasa mbele ya klabu ya Chelsea.ConteKlabu ya Tottenham imekua kwenye ubora katika michezo yake miwili ya mwisho na kufanikiwa kujisimika kwenye nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Huku wakiisogelea kwa karibu klabu ya Manchester United inayokamata nafasi ya tatu.

Acha ujumbe