Klabu ya Yanga imefanikiwa kupata alama moja ugenini katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya klabu ya Real Bamako ya nchini kwa matokeo ya bao moja kwa moja.

Yanga ambao walitangulia kupata bao katika mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wake matata Fiston Kalala Mayele dakika ya 60, Lakini wenyeji hawakua nyuma wakijitahidi kupeleka mashambulizi ya hapa na pale mpaka wakafanikiwa kusawazisha bao dakika ya 90 ya mchezo.yangaKlabu ya Wananchi walikua na nafasi kubwa ya kuweza kuandika rekodi siku ya leo kupitia mchezo huo dhidi ya Real Bamako kama tu wangefanikiwa kupata alama tatu, Klabu hiyo ingefanikiwa kufikisha alama 6 kwenye michuano ya kombe la shirikisho kwa mara ya kwanza.

Yanga sasa wamefanikiwa kufikisha alama 4 katika kundi lake wakiwa nafasi ya pili kwenye kundi hilo ambalo linaongozwa na Us Monastir wenye alama 7 mpaka sasa, Hivo vijana wa Profesa Nabi wako kwenye nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya robo fainali.yangaKlabu ya Yanga bado ina michezo mitatu mkononi kwakua tayari imeshacheza michezo mitatu ikifanikiwa kushinda mmoja, sare moja, na kufungwa mchezo mmoja Hivo klabu hiyo ina alama tisa za kuzipambania katika michezo mitatu iliyobakia na kuweza kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho.

 JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa