Klabu ya Yanga itakua ikisaka rekodi leo nchini Mali katika mchezo wake wa tatu wa hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Afrika wakicheza na klabu ya Real Bamako kutoka nchini humo.
Klabu ya Yanga ikifanikiwa kupata alama tatu katika mchezo wa kombe la Shrikisho leo dhidi ya Real Bamako watakua wanafikisha alama sita, Hivo kuwafanya kuweka rekodi ya kufikisha alama sita kwa mara ya kwanza katika makundi ya michuano hiyo barani Afrika.Klabu ya Wananchi ilifanikiwa kupata alama tatu muhimu katika mchezo wa pili wa kombe la shirikisho waliocheza katika uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Tp Mazembe wikiendi iliyomalizika, Hivo kushinda mchezo wa leo dhidi ya Real Bamako utawafanya kuandika historia mpya.
Klabu ya Yanga wamekua kiwango bora msimu huu katika michuano ya Afrika na kushinda ugenini kwao ni jambo linalowezekana, Kwani mchezo ambao uliwafanya kufuzu hatua ya makundi katika kombe la shirikisho walishinda ugenini dhidi ya klabu ya Club Africain kutoka Tunisia.Katika awamu tatu za mwisho wakati klabu ya Yanga inashiriki michuano ya kombe la Afrika hatua ya makundi haijawahi kufikisha alama 6 huku alama nyingi ambazo walivuna zilikua alama 4, Hivo leo Wananchi wana nafasi kubwa ya kuandika rekodi mpya kama wakifanikiwa kupata ushindi dhidi ya Real Bamako.