Klabu ya Inter Milan imepoteza mchezo leo katika ligi kuu ya Italia Serie baada ya kukubali kichapo cha bao moja kwa bila dhidi ya klabu ya Bologna iliyokua nyumbani katika dimba lake la Renato Dell’Arra.
Klabu ya Inter Milan hawapo kwenye kiwango bora tangu kuanz akwa msimu huu kwani klabu hiyo imekua ikipata matokeo kwa kusuasua katika michezo yake, Bologna wao wakiendeleza kile ambacho kimekua kikiwasibu mabingwa hao wa zamani wa ligi hiyo.Klabu ya Bologna walionekana kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu na kuzuia kwa umakini mkubwa huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza, Mpaka pale dakika ya 76 Riccardo Orsolini alipoipatia bao la ushindi Bologna na kufanikiwa kuibuka na alama zote tatu.
Inter Milan ambao wametoka kushinda katikati ya wiki mchezo wao wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Fc Porto kwa goli moja kwa bila wameendelea na shida yao ya kushindwa kufunga magoli, Kwani mchezo wa leo wamefanikiwa kupiga mashuti manne yaliyolenga lango bila kupata goli hata moja.Licha ya kupoteza katika mchezo wa leo dhidi ya klabu ya Bologna Inter Milan wameendelea kusalia katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu nchini Italia wakifiwa na alama zao 47, Lakini matumaini ya ubingwa kwa klabu hiyo ni madogo sana kwani wameachwa kwa jumla ya alama 18 na vinara wa ligi hiyo klabu ya Napoli.