Klabu ya Tottenham Hotspurs imefanikiwa kufuta uteja kwa klabu ya Chelsea baada ya kuinyuka kwa mabao mawili kwa bila katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa katika dimba la Spurs.

Tottenham wamekua wakipata matokeo yasiyovutia pale ambapo wanakutana na klabu ya Chelsea, Lakini leo katika mchezo huo wa London Derby vijana wa Antonio Conte walikataa kua wateja wa klabu ya Chelsea kwani waliweza kuifunga klabu hiyo kwa mabao mawili kwa sifuri na kuchukua alama zote tatu.TottenhamKlabu ya Chelsea nayo imeendelea kua kiwango kibovu na leo inatimiza mchezo wa 15  wakiwa wamefanikiwa kupata ushindi kwenye mchezo mmoja tu, Klabu hiyo ipo kwenye wakati mgumu zaidi zaidi ni kocha wa klabu hiyo Graham Potter ambaye amekua akiandamwa sana kutokana na matokeo mabovu ya timu hiyo.

Tottenham ambao kabla ya mchezo wa leo walifanikiwa kucheza michezo tisa ya kimashindano dhidi ya klabu ya Chelsea na kushindwa kupata matokeo ya ushindi, Lakini leo magoli ya Oliver Skipp na Harry Kane yaliwafanya kuondoa rekodi hiyo mbuvu dhidi ya Chelsea.TottenhamKlabu ya Tottenham baada ya kuchukua alama tatu za leo mbele ya klabu ya Chelsea wanaendelea kujiimarisha katika nafasi ya nne baada ya kufikisha alama 45, Huku wakiipumulia klabu ya Manchester United waliopo nafasi ya tatu na alama zao 49.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa