Potter: Mimi Ndio Natakiwa Kuwajibika

Kocha wa klabu ya Chelsea Graham Potter amesema matokeo mabovu ambayo klabu ya Chelsea inaendelea kuyapata kwasasa yeye ndio anatakiwa kuwajibika na sio wachezaji wake.

Kocha Potter wakati anazungumza na wanahabari punde baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi yao na klabu ya Tottenham ambapo wamefungwa mabao mawili kwa bila, Amesema hali mbaya ya matokeo inayoendela ndani ya klabu ya Chelsea yeye kama kocha ndio anatakiwa kuwajibika.PotterKlabu ya Chelsea ambayo imecheza michezo 15 ya kimashindano ambapo wameambulia kushinda mchezo mmoja tu kati ya michezo yote hiyo, Hali hii inaonesha ni kwa namna gani klabu hiyo inapitia wakati mgumu huku leo wakidondosha alama zingine tatu dhidi ya mahasimu wao klabu ya Tottenham.

Baada ya mchezo dhidi ya Tottenham kocha Potter ameeleza kua wachezaji wake wanajitoa kwa kila kitu kiwanjani na wanaumizwa na matokeo haya, Lakini akaendelea kusisitiza kua yeye ndio atawajibika kutokana na haya ambayo yanaendelea ndani ya klabu hiyo.PotterKocha Potter mpaka sasa inaonekana viatu vya kocha aliyepita klabuni hapo Thomas Tuchel vimempwaya, Kwani tangu amejiunga na klabu ya Chelsea hajafanikiwa kubadilisha chochote kwenye klabu hiyo zaidi timu hiyo inaonekana ndio inaendelea kudidimia ikiwa chini yake.

Acha ujumbe