Tottenham Yambeba Danjuma Kibabe

Klabu ya Tottenham Hotspurs imefanikiwa kumchukua mshambuliaji wa klabu ya Villarrela ya nchini Hispania Arnaut Danjuma kwa mkopo wa miezi sita mpaka mwisho wa msimu huu.

Tottenham imefanikiwa kumchukua mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi kwa mkataba wa mkopo wa nusu msimu, Hivo mshambuliaji huyo atawatumikia majogoo hao wa jiji la London mpaka mwishoni mwa msimu huu huku kukiwa hakuna kipengele cha kumnunua jumla mchezaji huyo.tottenhamArnaut Danjuma alifanikiwa kufanya vipimo vya afya na klabu ya Everton mwishoni mwa wiki iliyomalizika lakini Klabu ya Tottenham ilifanikiwa kupindua meza dili hilo na kumchukua mshambuliaji huyo, Everton wamepokonywa tonge mdomoni na vijogoo hao wa London.

Klabu ya Tottenham imekua haifanyi vizuri kunako ligi kuu ya Uingereza hivo walihitaji kuingia sokoni ili kuhakikisha wanaimarisha timu hiyo, Kocha wa klabu hiyo Antonio Conte ameeleza mara kadhaa kua timu hiyo inahitaji kuongeza wachezaji wenye ubora ili kuweza kushindana katika michuano mbalimbali wanayoshiriki.tottenhamSpurs bado wapo sokoni kutafuta wachezaji wenye ubora zaidi ili kuweza kuimarisha timu hiyo ambvayo imeonekana kudorora mpaka sasa, Kocha Antonio Conte amekua akihitaji kupatiwa wachezaji wenye ubora mkubwa mara kadhaa ili kuifanya klabu hiyo kua shindani na sio timu inayoshiriki kwenye michuano mbalimbali.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.