Kiungo fundi wa klabu ya Brighton Hove and Albion Moises Caicedo amesema kua akili yake kwasasa ipo ndani ya klabu hiyo na taarifa ambazo zinazungumzwa nje hazimpi tatizo.
Kiungo Moises Caicedo anatajwa sana kuondoka ndani ya klabu ya Brighton na klabu ya Chelsea ni moja ya klabu zinazoelezwa zaidi kuhitaji saini ya kiungo huyo, Lakini mchezaji huyo ameweka wazi kua hana mpango wa kuondoka ndani ya klabu hiyo.
Kiungo huyo ameendelea kusisitiza kua akili yake kwasasa ipo ndani ya Brighton kwakua klabu hiyo inampa nafasi ya kucheza kila wikiendi, Hivo hajioni akiwa nje ya klabu hiyo siku za hivi karibuni kama ambavyo taarifa zimekua zikienea kua anaondok klabuni hapo.
Caicedo amekua kwenye ubora mkubwa kwenye klabu ya soka ya Brighton na kua moja ya viungo bora wa ulinzi kwenye ligi kuu ya Uingereza, Hivo imemfanya kua moja ya viungo wanaotazamwa na kufatilia zaidi na vilabu mbalimbali kwenye ligi kuu ya Uingereza.
Klabu ya Brighton wenyewe hawana mpango wa kumuachia mchezaji huyo kwenye dirisha dogo la mwezi Januari, Lakini pia mchezaji huyo ameonesha anahitaji kusalia ndani ya klabu hiyo kutokana na fursa klabu hiyo inayompatia ya kucheza kila wikiendi kama ambavyo ameeleza yeye mwenyewe.

