Kocha wa klabu ya Brighton Hove and Albion Robero De Zerbi amesema kiungo wake Moises Caicedo bado yupo sana ndani ya timu hiyo na hawatarajii kumuuza dirisha hili la mwezi Januari.

Klabu ya Chelsea ambayo imekua ikifanya usajili mara kwa mara kwasasa inaelezwa kua inamfatilia kiungo Moises Caicedoanayekipiga Brighton, Ndipo kocha Roberto De Zerbi akaeka wazi kua mchezaji huyo hauzwi kwasasa ndani ya timu hiyo.de zerbiKocha raia wa Italia ambaye amejiunga na klabu hiyo akichukua mikoba ya aliyekua kocha wa timu hiyo Graham Potter amefanikiwa kuendelea kuiimarisha timu hiyo, Na mchezaji Moise Caicedo ameendelea kua moja ya wachezaji muhimu ndani ya timu hiyo.

Kiungo wa kimataifa kutoka Ecuador Moises Caicedo amekua moja ya wachezaji muhimu sana ndani ya klabu ya Brighton kuanzia kwa kocha Potter na mpaka sasa mwalimu De Zerbi, Hivo itakua ngumu kumuachia mchezaji huyo akaenda timu nyingine.de zerbiKocha Roberto De Zerbi anaelewa kua mchezaji huyo anaweza akaondoka timu hiyo kwenye dirisha kubwa majira ya kiangazi, Lakini msisitizo wake mkubwa ni mchezaji huyo kusalia kwenye timu hiyo mpaka mwisho wa msimu huu na kama ikitokea akaondoka kwenye timu hiyo dirisha kubwa ni sawa lakini sio dirisha hili dogo la mwezi Januari.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa