Klabu ya KMC imepoteza mchezo wa leo kwa bao 3-1 mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dsm, na kuwafanya KMC kupoyeza alama tatu muhimu ambazo wangezipata zingewafanya kupanda nafasi za juu kwenye msimamo.
Magoli yote matatu ya Namungo yalifungwa na mchezaji mmoja, Ibrahim Mkoko mawili kipindi katika kipindi cha kwanza na moja katika dakika za lala salama.
Kelvin Kijiri mnamo dakika 68 aliisawazishia KMC na kuwapa matumaini ya ushindi wakusanya ushuru wa Kinondoni, lakini dakika kadri zilivyozidi kwenda timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu na kuwafanya KMC kupoteza mchezo.
Matokeo haya yameifanya KMC kuwa nafasi ya 10 kwa alama 23, huku Namungo akiwa nafasi ya 5 na alama zake 26.

