Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Antonio Conte ameionya klabu ya Ac Milan baada ya ushindi wa goli moja kwa bila dhidi Spurs kua wanaweza kupindua meza kwenye mchezo wa pili watakapokutana jijini London na kuweza kufuzu hatua ya robo fainali.
Klabu ya Tottenham Hotspurs jana ilipoteza mchezo wake wa mkondo wa kwanza wa ligi ya mabingwa ulaya hatua ya 16 bora kwa bao moja kwa bila dhidi ya Ac Milan katika dimba la San Siro, Lakini Conte anaiona Tottenham ikiweza kufanya vizuri zaidi kwenye mchezo wa pili utakaopigwa katika dimba la Tottenham jijini London.
Klabu ya Tottenham bado ina nafasi ya kuweza kufuzu hatua ya robo fainali kama anavyoamini kocha wa klabu hiyo, Kwani wanaweza kupata matokeo ya ushindi katika dimba lao la nyumbani kwakua mzigo waliopewa na Ac Milan sio mzito sana hiyo ni baada ya kupoteza kwa bao moja kwa bila.
Kocha Antonio Conte amekiri kua alitarajia ushindani dhidi ya Ac Milan katika dimba la San Siro kwani siku zote anajua kucheza katika uwanja huo sio jambo jepesi, Lakini aliwapongeza wachezaji wake kutokana na kiwango walichoonesha vilevile akiwapongeza Milan kwa kuzuia vizuri pale walipotengeneza nafasi za kufunga lakini zikazuiliwa.
Antonio Conte pia ameridhishwa na uwezo wa wachezaji wake wawili wailoocheza katika nafasi ya ulinzi siku ya jana ambao ni vijana wadogo ni Pape Sarr na Skippy akisema wamelipa imani ambayo aliweka kwao, Hivo anatarajia kuona makubwa zaidi kutoka kwao.

