Klabu ya Manchester United inaelezwa ipo mbioni kununuliwa na waarabu kutoka nchini Qatar wakiongozwa na Skeikh Jassim Emir Al Thani ambaye ndio ataongoza ununuzi wa klabu akiwa kama mwekezaji mkuu.
Klabu ya Manchester United imekua chini ya familia ya Glazers kutoka nchini Marekani tangu mwaka 2005 huku wakihakikisha klabu inafanikiwa kwa kiwango kikubwa kabla ya kuonekana kufeli hatua za mwisho, Huku mashabiki wa klabu hiyo kuwataka kuachia timu hiyo.
Familia ya Glazer ilitangaza kuiuza klabu hiyo mwishoni mwa mwaka jana baada ya maandamano ya muda mrefu ya mashabiki wa klabu hiyo, Huku mahojiano ya Ronaldo na Piers Morgan yakichochea wamiliki hao kuiachia Manchester United baada ya kugundulika kua wamiliki hao hawazingatii kuhusu miundombinu ya klabu hiyo.
Sheikh Jassim inaelezwa mpaka sasa ndio anaongoza kwa ofa kubwa akimshinda kwa mbali mpinzani wake Jim Ratcliff ambaye nae alikua ameweka ofa ya kuinunua klabu hiyo, Lakini tajiri huyo kutoka Qatar ameonekana kua na ofa nzuri ambayo imewashawishi Glazers kuweza kumuachia timu hiyo.
Sheikh Jassim inaelezwa ameahidi kununua klabu hiyo na kuchukua hisa zote kutoka wadau wengine ambao wana hisa kwenye, Lakini pia amesema atahakikisha anafuta madeni yote ya klabu hiyo ambayo imekua ikidaiwa kwa muda mrefu bila kusahau ahadi yake ya kuboresha miundombinu ya klabu hiyo.

