Yanga Yafa Kiume kwa Mkapa

Klabu ya Yanga imekubali kipigo cha mabao mawili kwa moja katika dimba la nyumbani Benjamin William Mkapa dhidi ya USM Algier kutoka nchini Algeria katika fainali ya kwanza ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Klabu ya Yanga ilikubali bao kipindi cha kwanza lilifungwa na mshambuliaji Aymen Mahious dakika ya 32 ya mchezo na kuwapa uongozi USM Algier, Klabu hiyo imekua ilienda kipindi cha kwanza ikiwa inaongoza bao moja mbele ya Wananchi.YangaKipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa vijana wa kocha Nabi ambapo walikua wakifanya mashambulizi mara kwa mara na kujaribu kutafuta bao la kusawazisha, Lakini USM Algier walikua makini sana katika kuhakikisha Wananchi hawapati bao katika mchezo huo.

Yanga hawakua nyuma waliendelea kushambulia mara kwa mara kwenye lango la USM Algier mpaka pale ambapo watapata bao la kusawazisha, Mnamo dakika 82 ya mchezo Fiston Kalala Mayele aliwasawazishia bao Wananchi na kufufua matumaini kwa Wananchi.YangaYanga walijikuta wanaruhusu bao la pili ndani ya dakika mbili baada ya kusawazisha bao namchezo kumalizika USM Algier kushinda kwa mabao mawili kwa moja, Hivo kuwapa mtihani mzito kuelekea mchezo wa marudiano wa fainali utakaopigwa nchini Algeria wiki ijayo ambapo watakua na kazi nzito ya kufanya ili kutwaa ubingwa huo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.