Klabu ya Arsenal imefanya mauaji katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Uingereza msimu wa mwaka 2022/23 baada ya kuibamiza Wolverhampton kwa mabao matano kwa bila Huku Man United wao wakimaliza nafasi ya tatu.
Arsenal leo walipigilia msumari katika nafasi yao ya pili baada ya kushinda kwa mabao matano kwa bila wakiwa katika dimba la la nyumbani la Emirates, Mabao yao yakifungwa na Granit Xaka aliefunga mabao mawili, Gabriel Jesus, Bukayo Saka, pamoja na beki Jakub Kiwior.
Vijana hao wa Mikel Arteta wanafanikiwa kumaliza msimu wakiwa ndani ya nafasi nne za juu ikiwa ni baada ya miaka saba kupita, Hivo msimu huu umekua wa mafanikio kwa Arsenal japokua wamehuzunika kwa kiwango fulani baada ya kuteleza mwishoni na kuukosa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza na kubebwa na Manchester City.
Manchester United wao wakiwa katika dimba lao la Old Trafford waliweza kupata matokeo ya ushindi wa mabao mawili kwa moja, Huku wakihakikisha wanamaliza wakiwa nafasi ya tatu mabao ya Man United yalifungwa na Jadon Sancho na Bruno Fernandes huku bao la kufutia machozi la Fulham likifungwa na Kenny Tete.
Manchester United wao wamekua na msimu bora sana chini ya kocha Erik Ten Hag ambaye ndani ya msimu wake wa kwanza ndani ya klabu hiyo amefanikiwa kutwaa taji moja la Carabao, Akiwa anasubiri kucheza fainali nyingine ya FA vilevile akiwa ameirudisha klabu hiyo kwenye ushiriki wa ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao.

