Winga hatari wa kimataifa wa Argentina Angel Di Maria ambaye alikua anakipiga ndani ya klabu ya Juventus inayoshiriki ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A anatimka ndani ya timu hiyo kama mcheza huru.
Angel Di Maria alisaini mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu ya Juventus akitokea kwa mabingwa wa Ufaransa klabu ya PSG katika majira ya joto mwezi Juni mwaka jana, Lakini mchezaji huyo ametangaza kutimka klabuni hapo mara moja kama mchezaji huru na mpaka sasa haijafahamika ataenda klabu gani.
Winga huyo wa kimataifa wa Argentina amekua kwenye ubora mkubwa sana ndani ya klabu ya Juventus licha ya timu hiyo kutofanya vizuri msimu huu katika michuano ambayo wameshiriki, Vilabu kadhaa vinaelezwa kumnyemelea mchezaji huyo lakini ikiwa hajaweka wazi mpaka sasa anaelekea timu gani.
Klabu ya Benfica ambayo ndio timu ya kwanza ya Angel Di Maria kucheza barani ulaya baada ya kutoka nchini kwao Argentina ina matumaini ya kumrudisha mchezaji huyo katika viunga vya Estadio da Luz, Lakini mpaka sasa hakuna tamko rasmi juu ya wapi mchezaji huyo atatimkia.
Vyanzo mbalimbali pia vinaeleza kua huenda Di Maria akaungana na magwiji wengine kuelekea Saudia Arabia ambapo mastaa wengi sana wanakimbilia huko, Kwani hivi karibuni Karim Benzema ameondoka ndani ya Real Madrid na kutimkia huko hivo inawezekana na mchezaji huyo akaungana na magwiji wengine nchini humo.

