West Ham imeshtakiwa na UEFA kufuatia tabia ya mashabiki wao wakati wa ushindi wao wa fainali ya Ligi ya Europa Conference dhidi ya Fiorentina katikati ya wiki.

Nahodha wa timu hiyo ya Serie A, Cristiano Biraghi alijeruhiwa kichwa baada ya kugongwa na kikombe kimoja cha plastiki alichorushiwa kutoka mwisho kikiwa na wafuasi wa West Ham alipoenda kupiga kona kipindi cha kwanza.
West Ham pia wameshtakiwa kwa uvamizi wa uwanja wa michezo. Klabu hiyo ya Italia imepata mashtaka mawili yanayohusiana na kuwasha fataki na kurusha vitu.

Bodi ya Udhibiti, Maadili na Nidhamu ya UEFA (CEDB) itaamua kuhusu suala hilo kwa wakati ufaao.

