Kiungo wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba ambaye amewahi kukipiga klabu ya Manchester United huenda akafikia mwisho ndani ya klabu hiyo.
Vyanzo mbalimbali kutoka nchini Italia vinaeleza kua mchezaji huyo huenda Pogba akaondoka Juventus kwenye dirisha hili, Huku ikielezwa Juventus ndio inatoa kipaumbele kuachana na mchezaji huyo.
Mchezaji huyo amekua akiandamwa na majeraha ndani ya klabu ya Juventus tangu amejiunga mwishoni mwa msimu uliopita akitokea Man United, Hivo kukosekana kwake uwanjani kumeifanya Juventus kuachana na mchezaji huyo.
Wababe hao wa soka nchini Italia wanataka kuachana na Pogba kutokana na kutokuwepo uwanjani mara kwa mara, Hivo jambo ambalo wanalifikiria ni kukaa chini na mchezaji huyo na kuangalia namna ambayo wataweza kumalizana.
Paul Pogba inaelezwa amepokea ofa tofauti tofauti kutoka vilabu vya Saudia ambavyo vimeonesha kuhitaji huduma yake, Huku klabu ya Juventus wao watahitaji kiasi cha Euro milioni 10 tu ili kumuachia kiungo huyo kama timu itakuja na ofa.

