Manchester United Kukipiga na Lyon

Klabu ya Manchester United itashuka dimbani leo katika mchezo wake wa pili wa kujiandaa na msimu mpya kukipiga na klabu ya Olympique Lyon nchini Scotland.

Manchester United watakua nchini Scotland ambapo ndio watacheza mchezo wao wa mwisho kabla ya kwenda nchini Marekani ambapo ndio watakua na michezo yote ya maandalizi ya msimu kuelekea msimu ujao.manchester unitedMashetani Wekundu leo watakua wanatafuta ushindi wao wa pili katika michezo ya kujiandaa na msimu, Kwani mchezo wa kwanza walifanikiwa kupata ushindi wa mabao mawili dhidi ya klabu ya Leeds United ambayo ilishuka daraja kwenye ligi kuu ya Uingereza.

 

Manchester United katika mchezo wa leo wanatarajiwa kua na wachezaji wao wa kikosi cha kwanza ambao hawakua wamejiunga na timu hiyo katika mchezo wa kwanza ambao ni Marcus Rashford, Antony, Dalot, Maguire, Shaw, Lindelof,pamoja na Bruno Fernandes.manchester unitedKlabu ya Manchester United baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Lyon leo wataelekea nchini Marekani ambapo watamalizia michezo yao ya kujiandaa na msimu mpya na vilabu vikubwa kama Real Madrid, Arsenal,pamoja na klabu ya Borussia Dortmund.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.