Donny Van De Beek Arejea na Goli Man United

Kiungo wa klabu ya Manchester United Donny Van De Beek amefanikiwa kucheza mchezo wake wa kwanza na klabu hiyo baada ya kutoka kwenye majeraha na kufanikiwa kufunga bao.

Klabu ya Manchester United ilikua na mchezo wa kirafiki leo dhidi ya Olympique Lyon ambapo wameshinda bao moja kwa bila, Huku kiungo Donny Van De Beek ambaye ametoka kwenye majeraha ndio alifunga bao pekee la klabu hiyo.donny van de beekKiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi amekua hana wakati mzuri sana ndani ya klabu ya Manchester United tangu ajiunge mwaka 2020, Kwani amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara na kuepelekea kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Donny Van De Beek amezungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo na kuonesha kufurahishwa kurudi uwanjani baada ya miezi sita, Lakini pia akifurahia kufunga bao pekee ambalo limeipa ushindi klabu yake.donny van de beekKiungo Donny Van De Beek taarifa zinaeleza klabu hiyo inataka kumuuza katika majira haya ya joto kama kuna klabu itaweza kufika kiwango ambacho wanakihitaji, Kwani kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji ambao wamewekwa sokoni na klabu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.